Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiwe vya kahawa kutumika uhamasishaji chanjo

Kijiw Ed Vijiwe vya kahawa kutumika uhamasishaji chanjo

Fri, 1 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

WATU wa uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19 mkoani Kigoma wameshauriwa kutumia vijiwe kama vya kahawa kwenda kutoa mada na kujibu maswali yanayo watatiza wananchi kuhusu chanjo.

Ushauri huo umetolewa wakati wa kikao cha uhamasishaji wa masuala ya chanjo yaliyo husisha makundi mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari, viongozi wa dini, wafanyabiashara na makundi mengine.

Antony Kayanda mwandishi wa habari amesema uhamasishaji unaoendelea mkoani humo umekuwa ukiegemea zaidi maeneo ya barabarani tu lakini kuna fursa ya utoaji elimu ambayo bado hawajaifanyia kazi.

Ameshauri ni vyema yakatumika maeneo yenye mikusanyiko ya kutosha ambapo moja ya eneo hilo ni meza ya duara ambalo limekuwa likitumiwa na wakazi wa Kigoma kujadili mada mbalimbali za kijamii, kisiasa na michezo.

"Yapo maeneo yenye mikusanyiko ya kutosha lakini tangu harakati hizi zianze sijaona yakifikiwa" Amesema.

Mganga Mkuu Mkoa wa Kigoma Simon Chacha, amesema kila ushauri wenye tija wanaupokea na wanatarajia kufikia maeneo yote ili kuhakikisha kila mtu anapata elimu hiyo na kupata majibu ya maswali yanayo mtatiza.

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye, amesema kuna haja ya kuyatumia makundi ya watu wanao hudumia watu wengi katika ufikishaji wa elimu hasa vijiweni .

Ameeleza endapo watapatiwa elimu ni rahisi kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe itaeahisisha kulipokea jambo hilo na kuongeza idadi ya walio kubali kuchanja kwa hiari.

Chanzo: ippmedia.com