Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji vyote 450 Manyara kupatiwa umeme

Umeme Ms Vijiji vyote 450 Manyara kupatiwa umeme

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati zaidi ya vijiji 10,000 kati ya vijiji 12,318 nchini vimeshapatiwa nishati ya umeme, vijiji vyote 450 vya Mkoa wa Manyara, vitapatiwa umeme mwishoni mwa mwaka huu wa 2023.

Mwenyekiti wa bodi ya wakala wa nishati vijijini (Rea) meja jenerali mstaafu Jacob Kingu ameyasema hayo, Novemba 9 baada ya kutembelea mradi wa kuongeza nguvu nishati ya umeme Darakuta wilayani Babati mkoani Manyara.

Kingu amesema ameridhishwa na namna Rea inavyosambaza nishati ya umeme kwani vijiji vyote 450 vya Manyara vitapatiwa umeme hadi mwishoni mwa mwaka huu wa 2023.

Amesema Rea imepiga hatua kubwa kwani zaidi ya vijiji 10,000 kati ya 12,318 sawa na asilimia 90 ya vijiji vyote nchini hadi ifikapo Desemba mwaka 2024 vitafikiwa na umeme.

"Bodi yangu kwa kweli imeridhishwa na Rea kwa kushirkiana na wadau wa maendeleo kutoka nje ya nchi na taasisi za kimataifa za fedha kwa kuwezesha usambazaji wa umeme kwa asilimia 90 hapa nchini," amesema Kingu.

Amesema Rea inatarajia kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini kabla ya kumalizika mwaka 2024, na kuwezesha watu wenye miradi kuwasilisha maombi yao katika bodi ili wapate nafasi ya kurahisisha upatikanaji wa nishati nchini.

"Nachukua nafasi hii kuwapongeza Rea kwa kazi nzuri ya kuhakikisha umeme unawafikia vijijini wakishirikiana na Tanesco kwani umeme unaozalishwa unaunganishwa kwao, amesema Kingu.

Amesema mradi mdogo wa nishati jadidifu wa Darakota unapaswa kuwepo maeneo mengi nchini kwani unaongeza nguvu katika usambazaji wa nishati ya umeme.

Mkurugenzi msaidizi ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) Enock Nyanda ameitaka jamii kusaidia wawekezaji wa sekta ya nishati katika kukabiliana na shughuli zote zinazosababisha kuharibu misitu na vyanzo vya maji.

Mkurugenzi huyo anayeshughulikia fursa za uzalishaji na uchumi amesema serikali inawezesha upatikanaji wa nishati hasa vijijini ili kusaidia kasi ya ukuaji wa uchumi.

"Kwa kweli naisihi jamii nchini iweze kubadilika kwa kusaidia wawekezaji wa sekta ya nishati katika kukabiliana na shughuli zote zinazosababisha kuharibu misitu na vyanzo vya maji vinavyotuzunguka," amesema Nyanda.

Mkurugenzi wa mtambo mdogo wa kuzalisha umeme Darakuta, Ritha Bapst amezitaja baadhi ya sababu ambazo ni hatarishi kwa uzalishaji wa nishati hiyo ni uharibifu wa mazingira na kufanya shughuli za kijamii karibu na eneo hilo.

Bapst ametaja matukio mengini ni kutokana na kuchoma misitu, kufanya shughuli nyingine za kijamii kwenye vyanzo vya maji vitendo ambavyo ni hatari kwa uzalishaji nishati hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live