Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji vya Madaba vyataka maji

F8a1030f670fcc3e66b88a79796b10e8 Vijiji vya Madaba vyataka maji

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WANANCHI wa vijiji vya Lituta na Kipingu Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma, wameiomba serikali iwafikishie huduma ya maji katika makazi yao ili kumaliza kero yao ya maji muda mrefu kwani kwa sasa wanalazimika kutumia maji ya visima vya asili vinavyotumiwa pia na wanyamapori.

Walisema licha ya kujengwa kwa miradi ya maji ikihusisha matenki yaliyojengwa kwenye vijiji hivyo, lakini mpaka sasa maji hayajasambazwa kwa wananchi.

Wananchi hao walitoa kilio chao mbele ya Mkuu wa wilaya ya Songea, Pololet Mgema, wakati alipofanmya ziara katika vijiji hivyo.

Hata hivyo Mkuu huyo wa wilaya alisikia kilio chao na kuagiza Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja maji yanasambazwa kwa wananchi kwani mradi huo wa maji umechukua zaidi ya miaka mitatu.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Anton Sanga akiwa katika ziara ya siku moja wilayani Songea kukagua utekelezaji wa miradi ya maji alisema wizara hiyo ina fedha za kutosha kwa ajili ya kujenga na kukamilisha miradi yote ya maji inayoendelea kutekelezwa na ile miradi viporo ambayo ujenzi wake umesimama kwa muda mrefu.

Chanzo: habarileo.co.tz