Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji elfu 10 vyafikiwa na umeme nchini kote

2a9e675b857e74afe75289861a659340 Vijiji elfu 10 vyafikiwa na umeme nchini kote

Sat, 13 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa amesema kuwa hadi kufikia Desemba mwaka jana Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini (REA) awamu ya tatu ulikuwa umefikia zaidi ya vijiji elfu 10 kati ya vijiji 12317 vilivyopo kote nchini .

Majaliwa amebainisha hayo leo Jijini Dodoma alipokuwa akitoa hotuba ya kuhairisha shughuli za Bunge na kubainisha kuwa ufikaji wa umeme katika vijiji hivyo ni sawa na 83.3%.

Aidha, Majaliwa amebainisha kuwa kwa mwaka huu Serikali imetanga Shilingi bilioni 171.9 ili kukamilisha usambazaji wa umeme katika vijiji vilivyobakia.

Chanzo: habarileo.co.tz