Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji 2,159 vilivyobaki kupata umeme

Ad53867d0382d420eb5e9b98c578b96a Vijiji 2,159 vilivyobaki kupata umeme

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI imesema itakamilisha kupeleka umeme katika vijiji vyote nchini na vilivyobaki vitakuwa vimepata nishati hiyo ndani ya miezi 18.

Kauli hiyo ilitolewa Bungeni Dodoma jana na Waziri wa Nishati, Dk Merdard Kalemani wakati akijibu swali na nyongeza la Mbunge wa Biharamulo, Ezra Chiwelesa (CCM).

Chiwelesa alitaka kujua ni lini serikali itakamilisha kupeleka umeme kutoka maeneo mbalimbali yakiwemo ya Geita kwenda Nyakanazi na maeneo mengine nchini.

DK Kalemani alisema tayari serikali imeshafikisha umeme katika vijiji vingi nchini, vilivyobaki 2,159 kati ya vijiji vyote 12,268 vitapata umeme ndani ya muda huo, vikiwemo vijiji katika Mkoa wa Geita. Maeneo ya Nyakanazi hadi Kigoma yatapata umeme.

Katika mkakati huo, pia katika umeme wa kujaziliza vijiji 32 vilivyobaki, kati yake vijiji saba vipo Biharamulo, vitapata umeme katika muda huo.

Naibu Waziri wa Nishati, Byabato akijibu swali la msingi la Chiwelesa alisema serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) inatekekeza mradi wa kituo kidogo cha Geita hadi Nyakanazi (KV 220) kutoka Rusumo na Geita. Utakapokamilika utaondoa tatizo hilo la kukatikakatika kwa umeme.

Mradi huu unahusisha ujenzi wa njia yakusafirisha umeme ya msongo wa kilovoti 220 kutoka Geita –Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 144.

Hadi sasa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme na kituo cha kupoza umeme, umefikia asilimia 60. Gharama ya mradi ni Euro milioni 45 sawa na takribani Sh bilioni 117.79. Mradi huo unatarajiwa kukamilika Machi 2021.

Chanzo: habarileo.co.tz