Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji 19 kunufaika na mradi wa Forvac wa uvuinaji endelevu wa misitu

9086609eed5ae0e94c9f0b43f0e66a0c Vijiji 19 kunufaika na mradi wa Forvac wa uvuinaji endelevu wa misitu

Wed, 31 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

VIJIJI 19 katika wilaya ya Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi vinatekeleza mpango wa usimamizi shirikishi wa hifadhi za misitu ya vijiji kwenye Mradi wa Forvac, unaofadhili usimamizi wa misitu kwa kuongeza mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu.

Mradi huo unatekelezwa na halmashauri husika na Shirika la Kuhifadhi Mipingo na Maendeleo (MCDI) na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).

Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa na mmoja wa watendaji katika vijiji vinavyotekeleza mradi huo,Husna Kijazi wilaya ya Ruangwa yenye vijiji 8 na Nachingwea vijiji 11, vina jumla ya hekta 66,756.52 za misitu chini ya hifadhi za misitu ya vijiji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashine inayotembea ya kuchakata magogo, kazi iliyofanywa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro; mtendaji huyo wa kijiji alisema kamati za maliasili kwa kushirikiana na halmashauri za wilaya hizo na wataalamu wa TFS na MCDI chini ya uwezeshaji wa Forvac wameshandaa mipango ya usimamizi na uvunaji ya misitu ya hifadhi ya vijiji 13.

Alisema vijiji ambavyo vimekamilisha mipango ya usimamizi na uvunaji huo ni Namatunu,Ngunichile, Mbondo, Kilimarondo, Kiegei B kwa wilaya ya Nachingwea na vijiji vya Nandenje, Lichwachwa,Nahanga, Ng’au, Mchichili, Mmawa na Malolo kwa wilaya ya Ruangwa.

Kwa mujibu wa Husna utekelezaji wa mpango huo umeleta mafanikio makubwa ikiwamo ujenzi wa ofisi za vijiji, ununuzi wa trekta ujenzi wa zahanati, madarasa na madawati

Aidha zaidi ya Sh milioni 50.2 zimewezesha ujenzi wa kituo cha Afya Ngunichile.

Pamoja na mafanikio hayo Husna alisema kuna changamoto kubwa katika uuzaji wa mbao na kutaka Serikali itoe kipaumbele kununua mazao ya misitu kutoka kwenye hifadhi ya vijiji vinavyotekeleza mradi huo wa hifadhi.

Programu ya Fovarc ilianza kutekelezwa mwaka 2018 na inafadhiliwa na serikali ya Tanzania na Finland.

Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera pamoja na Ilani ya Chama cha mapinduzi ambapo vijiji vimetakiwa kushiriki katika uhifadhi wa mazingira kwa kuwa na uvunaji endelevu wa mazao ya misitu.

Chanzo: www.habarileo.co.tz