Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji 11 vyakabidhiwa vyeti umiliki ardhi

Vijiji 11 vyakabidhiwa vyeti umiliki ardhi

Tue, 29 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Longido. Vijiji 11 Wilayani Longido mkoani, Arusha vimekabidhiwa vyeti vya umiliki wa  ardhi  na vyeti vya hakimiliki za kimila za maeneo ya pamoja ya nyanda za malisho ili kuepuka migogoro ya ardhi na kujikwamua na umaskini.

Vijiji vilivyopewa hati hizo ni Ilchang’itsangishu, Gilailumbwa, Loondowuo, Orkejuloongishuu, Armanie, Eworendeke, Matale, Amairowa, Karao,Sinonik na Kimwati.

Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya Longido, Toba Nguvila  jana Oktoba 28, 2019  amesema hati hizo zitasaidia kuepusha migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.

 Nguvila aliyemuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Frank Mwaisumbe, amesema vyeti na hati hizo zimekabidhiwa kwa vijiji ambavyo vipo tarafa tatu za Kitumbeine, Longido na Engarenaibo.

Amesema mradi huo wa miaka mitano, unaoelekea ukingoni mwishoni mwa mwaka huu, umefadhiliwa na shirika la “Ujamaa Community Resource Team.”

Amesema mradi huo unajumuisha Kata za Gilailumbwa, Meirugoi, Kimokouwa, Ketumbeine Engarenaibor na Kata ya Matale ambazo kwa pamoja wamefanikiwa mpango wa matumizi bora ya Ardhi kwa lengo la kulinda nyanda za malisho na ardhi kwa ujumla na kusimamia kwa uendelevu.

Pia Soma

Advertisement

Akisoma taarifa ya mradi huo, Ngalaikiti Laiser amesema mradi huo pia utasaidia kujenga uwezo wa wanavijiji juu ya usimamizi wa matumizi bora wa ardhi na utawala bora .

"Mradi huu pia utasaidia kuepusha migogoro mikubwa kama baina ya wafugaji kugombea malisho," amesema

“Tumekuwa na migogoro ya mipaka iliyodumu takribani miaka 30 na kushindwa kupata ufumbuzi kati ya kijiji cha Kitale B na wosiwosi na kukwamisha juhudi za maendeleo lakini sasa mgogoro unaelekea kuisha,” amesema.

Mkurugenzi wa Shirika la Ujamaa CommunityResource Team, (UCRT), MakkoSinandeu amesema mradi huo una faida kubwa kwani pia ni utekelezaji wa mradi wa maisha bora kwa akinamama wa jamii za Kimasai .

Amesema katika mradi huo, wanawake wameshirikishwa kikamilifu kuanzia mwanzo wa zoezi hilo hadi mwisho.

Amesema Shirika lake linaamini baada ya utekelezaji huo wanavijiji wataitumia ardhi kwa utaratibu na mpango maalum ili matumizi bora ya ardhi.

“Vyeti hivi vinaipa mamlaka Halmashauri za vijiji kusimamia ardhi kwa sheria namba 5 ya Mwaka 1999 na wananchi wanakaa na kupanga matumizi sahihi ya ardhi,” amesema

Awali Mratibu wa Mradi huo, Jamboi Baramayegu amesema mradi huo umetekelezwa na mashirika matano ya Kimataifa ya  ambayo ni VSF-B,IDP, Trias Tanzania, WFP na Enabel kwa kushirikiana na mashirika mengine tisa ya Kitanzania.

Amesema huo ulipewa jina la Mradi wa Maisha bora ni wa aina yake maana unajumuisha sekta nne muhimu kwa maisha ambazo ni ardhi na mifugo, Maji, Biashara na Lishe.

Baramayegu amesema miongoni mwa wafadhili wa mradi huo ni Serikali ya Ubelgiji ambayo imetoa zaidi ya sh 20 bilioni.

Programu ya  miradi ya longido ilianza Mwaka 2015 hadi 2019 wakati wakati Mradi wa Engishon, umefadhiliwa na   Serikali ya Uingereza kupitia Shirika la “African Initiative” na umeanza kutekelezwa mwaka 2019 na utafikia tamati 2021.

Chanzo: mwananchi.co.tz