Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijiji 11 kunufaika na mradi wa maji Lindi

Ruvu Chini Maji.jpeg Vijiji 11 kunufaika na mradi wa maji Lindi

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Zaidi ya shilingi Bilioni moja zinatarajiwa kutumika katika vijiji vipatavyo 11 kutoka Kata tatu Naipanga, Chiumbati na Rahaleo Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi vinatarajia kunufaika na mradi wa huduma ya maji safi na salama wa Naipanga.

Hayo yamebainishwa leo na Meneja wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilayani humo Mhandisi Sultan Ndoliwa wakati akizungumza na kuutambulisha mradi huo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Vijiji.

Mhandisi Ndoliwa amesema mradi wa Maji wa Naipanga upo katika kata ya Naipanga ipo katika kata za Naipanga, Chiumbati, Rahaleo na Stesheni

"Mradi huu unajengwa chini ya Mpango wa lipa kwa matokeo (Payment for Result-PforR ) na kusimamiwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA)," amesema Mhandisi Ndoliwa.

Aidha amesema Mradi wa Maji wa Naipanga utatekelezwa na Mkandarasi Broadway Engineering Co Ltd- Dar Es Salaam kwa gharama ya sh.bil.1,187,057,785 na VAT kwa muda wa miezi 12 na Utekelezaji wake unaanza rasmi Leo Agosti 22, Mwaka huu na kukamilika Agosti 22, 2024.

Mhandisi Ndoliwa ameongeza kuwa mradi unatarajia kutoa huduma kwenye Vijiji 11 vya Chiumbati shuleni, Chiwindi, Tandika, Luagala, Rahaleo, Maendeleo, Kilombelo, Naipanga, Nagaga, Joshoni na Chekeleni ambapo utahudumia watu wapatao 19,110 kwa kuzingatia ratiba ya mgawanyo wa Maji ya WANAWASA.

"Mradi una tenki la ujazo wa Lita 300,000 na uzio, vituo vya kuchotea maji vyenye sehemu 2 kila kimoja na Mtandao wa mabombawenye urefu wa kilometa 32,425," amesema Mhandisi Ndoliwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live