Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana watakiwa kuchangamika fursa

Kunenge Pwan.png Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Abubakar Kunenge

Thu, 23 Sep 2021 Chanzo: Channelten

Vijana wa mkoa wa Pwani wamelaumiwa kwa kutochangamkia fursa za kazi za viwandani zinazojitokeza ndani ya mkoa huo, hasa ikizingatiwa kwamba mkoa wa Pwani ni miongoni mwa mikoa ya kimkakati katika ujenzi wa viwanda hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametoa lawama hizo muda mfupi kabla ya kugawa miguu bandia kwa wenye mahitaji mia moja, ikiwa ni msaada uliotolewa na Kampuni ya Kamal Group, ambapo jumla ya walemavu wa miguu mia moja kutoka Pwani walinufaika na msaada huo.

Bwana Kunenge amesema katika ziara alizofanya kwenye viwanda mbalimbali mkoanu humo, amekuwa akipokea malalamiko kutoka kwa wamiliki wa viwanda hivyo kuwa vijana wa mkoa huo wamekuwa wakishindwa kufanya kazi kwenye viwanda hivyo kutokana na sababu mbalimbali alisosema hazina msingi.

Kwa upande wao, Kampuni ya Kamal Group imesema imejenga kiwanda cha kutengeneza miguu bandia, ikiwa ni wajibu wao wa kurudisha sehemu ya faida wanayoipata kwa jamii.

Wanufaika wa msaada huo wanasema kupitia miguu hiyo ya bandia walioipata kutoka Kampuni ya Kamal Group wameweza kurudishiwa uwezo wao wa kufanya kazi kwa zaidi ya asilimia themanini.

Misaada hiyo kutoka Kampuni ya Kamal Group pia imetolewa kwa mikoa ya Dodoma, Iringa na Dar es Salaam ambapo tangu mpango huo uanze zaidi ya miguu bandia elfu moja imeshatolewa kwa Watanzania wenye kuhitaji.

Chanzo: Channelten