Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana wataka maeneo rasmi ya biashara

Thu, 17 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kukosekana kwa maeneo rasmi ya vijana kufanya biashara kumechangia baadhi yao kushindwa kushiriki kutoa maamuzi ya shughuli za kiuchumi, hivyo kuna haja ya serikali na wadau kufanyia kazi eneo hilo.

Haya yalibainishwa jana Jumamosi Oktoba 12,2019, kwenye mdahalo ulioandaliwa na United Nations Association Tanzania (UNA), uliolenga kujadili ushiriki wa vijana katika kutoa maamuzi kwenye shughuli za maendeleo.

Aidha, washiriki wa mdahalo kutoka mashirika mbalimbali yasio ya kiserikali na sekta binafsi ambayo yanamilikiwa na vijana kwa pamoja walisema kuna haja ya uwepo wa maneno maalum ambayo vijana waweze kufanya shughuli za kiuchumi bila kua na vipingamizi kama kodi ya pango na huduma zingine za kijamii.

 Mshiriki kutoka shirika la DOT Trust, Diane Nsiima alisema uwepo wa maeneo rasmi ya vijana kufanyia shughuli zao za kiuchumi utarahisisha upatikanaji mikopo na mafunzo kwani  watakuwa kwenye eneo moja hivyo ni rahisi kupatikana.

"Kuhamasisha upatikanaji wa mafunzo rasmi ili kuwajengea vijana uwezo wa kufanya shughuli za kiuchumi haswa ikizingatia ujuzi halisi kwa kila shughuli," alisema

Kwa upande wake, mwakilishi kutoka shirika la Opportunity for Youth, Rahma Mwita alisema kijana anaposhirikishwa anaweza kuwasilisha na kusimamia utekelezaji wa masuala ya vijana kwa kuzingatia uhitaji kwa wakati huo.

Pia Soma

Advertisement
Aidha vijana wakipewa maeneo rasmi watakuwa na uwezo wa kutambua na kuchanganua  shughuli za kiuchumi kulingana na mazingira na kuzitilia mkazo ili kupunguza mgongano wa ki - maslahi kati ya mifumo iliyopo na ubunifu wa vijana.

Naye mratibu wa mradi wa kuchochea ushiriki wa vijana kwenye uamuzi kutoka UNA, Lucas Phidelis, alisema mdahalo huo ulikutanisha vijana zaidi ya 30 kutoka taasisi mbalimbali lengo ilikuwa ni kutoka na agenda ambazo zitawasilishwa serikalini na sekta binafsi.

Alisema vijana pia wameshauri kuundwa mfumo wa ufuatiliaji na uendelezaji shughuli za vijana haswa katika kila ngazi ya halmashauri.

Pia halmashauri zinatakiwa kubeba dhamana za mahitaji ya shughuli za vijana kama leseni za biashara na viambatanishi,

kutengeneza kwa sheria ndogondogo za wilaya zinazo tambua na kusimamia ukuaji wa shughuli za vijana katika kila halmashauri.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz