Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana wapigwa 'stop' matumizi ya gongo

Pombe0 Gongo Vijana wapigwa 'stop' matumizi ya gongo

Mon, 23 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pombe haramu aina ya Gongo, bangi na mirungi, vimetajwa kuathiri baadhi ya vijana katika eneo la Marangu,Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro na kuwafanya washindwe kufanya shughuli za kiuchumi na kuhudumia familia.

Hayo yamebainishwa wakati wa kikao cha baraza la umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) Kata ya Marangu Mashariki, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro, kilichoenda sambamba na utolewaji wa elimu ya uchumi pamoja na athari za ulevi.

Wakizungumza baadhi ya vijana wamesema pombe imeathiri vijana wengi na kuwafanya kushindwa kuhudumia familia na kuacha jukumu hilo kwa wanawake na hivyo kuliomba jeshi la polisi kuongeza nguvu katika udhibiti wa Gongo na bangi, ili kunusuru vijana na janga hilo.

Akizungumza katika Baraza hilo,Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Moshi Vijijini, Yuvenal Shirima amesema tatzo la ulevi wa kupindukia kwa baadhi ya vijana limeendelea kukua katika baadhi ya maeneo na kuliomba jeshi la polisi kushirikiana kwa karibu na jamii, kudhibiti utengenezaji na matumizi ya pombe haramu aina ya gongo ili kunusuri kizazi cha sasa na baadae.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live