Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana UVCCM watakiwa kuacha kuwa ombaomba

Frank Kunzenza M Kiti Frank Kunzenza

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: eatv.tv

Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Chato Frank Kunzenza amewataka vijana wanaounda jumuiya hiyo kuacha tabia ya kuombaomba vitu badala yake waanzishe miradi ya kujiingizia kipato ili waache kulaumu watu wanaoshindwa kuwapa wanachohitaji

Kunzenza amesema hayo kwenye kikao cha baraza la UVCCM kilichofanyika ukumbi wa mikutano wa chama hicho na kuwaasa vijana kutumia mikopo ya halmashauri ili kubadilisha hali zao za kiuchumi na kuacha kuwa tegemezi.

"Mimi nitakuwa mstari wa mbele sana kuhakikisha kama mwenyekiti wa vijana, kwanza nawasemea vijana lakini pia nawatetea katika yale mambo yanawahusu wao ikiwa ni pamoja ili waweze kuondoa utegemezi na kulalamika kutegemea ajira za serikali ilihali zipo fursa ambazo wanaweza wakazipata nje ya ajira zile za serikali", alisema Kunzenza.

Afisa uhifadhi wa wakala wa huduma za misitu (TFS) Sebastian Siyengo kutoka Shamba la Miti Silayo amewataka vijana kujiingiza kwenye shughuli za kilimo cha Miti kitakacho wakwamua kiuchumi.

"Wapande Miti kwa sababu ni moja ya chanzo cha mapato, hivyo wanapopanda Miti na kwa Sasa Miti inapofika umri wa miaka 18 wanavuna kwahiyo watajipatia kipato na kuweza kuendesha shughuli zao za kila siku na maisha ya kila siku", alisema Siyengo.

Chanzo: eatv.tv