Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana 67 kufunzwa matumizi ya sayansi

Fri, 28 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vijana 67 kutoka mikoa tofauti nchini wanatarajiwa kuhudhuria kambi ya siku nne ili kujifunza namna wanavyoweza kutumia sayansi katika shughuli mbalimbali.

Kambi hiyo itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Januari 1 hadi 5, 2018 imeandaliwa na Kampuni ya ProjeKt Inspire iliyolenga kutoa mwongozo wa kitaaluma kwa wanafunzi wa sekondari kupenda masomo ya sayansi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Desemba 28, 2018, Ofisa Ushauri na Ubunifu wa kampuni hiyo, Harvey Kadyanji amesema kambi hiyo italenga kuondoa dhana kwamba masomo ya sayansi ni magumu

"Vijana hawa tumewapata kupitia mchujo maalumu tulioufanya baada ya wao kutuma maombi yao. Tutawaamsha vijana kiakili ili waweze kufanya uchaguzi sahihi wa taaluma zinazowafaa,"  amesema

Katika kambi hiyo pia utatolewa ushauri wa namna ya kuendeleza vipaji vyao, ubunifu wa vitu mbalimbali walivyovifanya ili kuhakikisha malengo yao yanafikiwa.

Ofisa Masoko wa kampuni ya Nabaki Afrika, Mukiza Mushumba amesema mbali na kuwa wadhamini wa kambi hiyo pia hutoa fursa kwa wanafunzi kuanzia shule ya msingi kujifunza namna ya kutumia sayansi katika shughuli za kila siku.

“Watoto wengi wanakimbia kusoma sayansi, hesabu, uhandisi na teknolojia kwa kuhisi masomo magumu lakini ukiwapatia fursa ya kujifunza kwa vitendo inakuwa rahisi kwao kuvutiwa na kutamani kusoma ili wafanye mambo mazuri,” amesema Mushumba.



Chanzo: mwananchi.co.tz