Dodoma. Vijana 5,875 wamesajiliwa katika vyuo vya Don Bosco nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa programu ya Serikali ya ukuzaji ujuzi kupitia mafunzo ya uanagenzi.
Akizungumza leo Jumamosi Septemba 14 2019 katika uzinduzi wa mafunzo stadi za kazi kwa vijana na maadhimisho ya miaka 100 ya Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) , Mkuu wa Don Bosco Afrika Mashariki, Padri Babu Augustine amesema awamu ya kwanza walianza na vijana 3,000.
Amesema kuwa vijana waliomaliza mafunzo awamu ya kwanza asilimia 65 wameshapata kazi, asilimia 15 wamejiajiri wenyewe.
"Sasa hivi tumeshirikisha vyuo vingine katika kutoa mafunzo haya. Tunashukuru viwanda na kampuni zilizowasaidia wanafunzi hao katika mafunzo ya ufundi na hata kuwaajiri," amesema.
Amesema wanafunzi 5875 waliosajiliwa katika mafunzo hayo ya miezi sita watafanya mitihani Februari, 2020 kwenda katika viwanda na kampuni kwa muda wa miezi miwili kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
Padri Augustine ameshukuru Serikali kwa kuwawezesha kufanikisha mafunzo hayo yatakayowapa ujuzi katika sekta mbalimbali.
Pia Soma
- Mbosso funguka kuhusu mtoto wake
- VIDEO: Mbosso: Ndugu wa Boss Martha walinikana siku nyingi, hawajaanza leo
- Wazazi watakiwa kuwalea watoto katika maadili