Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana 4000 watarajia kunufaika na mafunzo ya kujiajiri na kuajiriwa

Veta Ed Vijana 4000 watarajia kunufaika na mafunzo ya kujiajiri na kuajiriwa

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: ippmedia.com

Makubaliano ya utekelezaji wa mradi huo yamesainiwa Juni 28, mwaka huu jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dk. Pancras Bujulu na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Korea (KOICA) nchini Tanzania, Kyucheol Eo.

Akizungumza wakati wa kutia saini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkazi wa KOICA nchini Tanzania, Kyucheol Eo, amesema kuwa serikali yake imetenga kiasi cha dola za kimarekani 5,300,000 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo na kwamba utatekelezwa kwa miaka mitatu kuanzia 2021 hadi 2023.

Amesema VETA itashirikiana kwa karibu na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Ujerumani (GIZ) katika utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha vijana wa kitanzania wananufaika na ukuaji wa uchumi katika sekta zinazotegemea ujuzi wa ufundi stadi.

“KOICA inafurahi kushirikiana na VETA kusaidia vijana nchini Tanzania kupata ajira ikiwa ni pamoja na kujiajiri ili waweze kutimiza ndoto zao. Tutashirikiana pia na GIZ kutekeleza mradi huu ambao utanufaisha moja kwa moja vijana 4,000, ambapo kati yao 1,400 ni wanawake,” amesema Kyucheol Eo.

Chanzo: ippmedia.com