Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana 150 watapeliwa Mwanza

Mutafungwa2 Ed Vijana 150 watapeliwa Mwanza

Sat, 23 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vijana zaidi ya 150 wametapeliwa na moja ya kampuni jijini Mwanza, ambapo wananchi katika mkoa huo wameiomba serikali kufanya ufuatiliaji wa karibu kwa makampuni baada ya kupewa usajili ili kuepukana na utapeli.

Baadhi ya wananchi hao katika jiji la Mwanza wameeleza kukerwa na utapeli unaofanywa na baadhi ya makampuni mkoani humo, ambayo hufanya biashara zake kwa njia ya mtandao na kuiomba serikali kufanya usimamizi ili kuyadhibiti yatakayobainika kutozingatia sheria.

Akieleza mwenendo wa matukio ya utapeli mkoani humo Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema wanachunguza moja ya kampuni mkoani humo linalosadikika kuwatapeli vijana zaidi ya 150.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live