Dar es Salaam. Majeruhi 6 kati ya 38 wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefariki dunia na kufanya idadi ya waliofariki hadi sasa kufikia 82
Majeruhi hao ni wa ajali ya moto iliyotokea Morogoro baada ya lori la mafuta kupinduka na kuwaka Moto.
Akitoa taarifa hiyo leo Agosti 14, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha amesema kwa sasa wamebaki majeruhi 32.
Kati ya majeruhi hao 17 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine 15 wakiendelea kupatiwa matibabu katika wodi ya Sewahaji.
Mkuu huyo wa mawasiliano amesisitiza watu kuendelea kujitokeza kuchangia damu kwa kuwa bado kuna uhitaji mkubwa.
“Wapo wanakuja na kutuletea vijana wa kuchangia damu, niwashukuru kwa hilo na niwasisitize wengine waendelee kuja, damu inahitajika sana,”amesema Aminiel
Habari zinazohusiana na hii
- DNA kutumika kutambua majeruhi ajali ya moto waliolazwa Muhimbili
- Dereva lori la mafuta lililoteketea kwa moto apatikana akiwa hai
- Majeruhi mwingine ajali ya Morogoro afariki, vifo vyafikia 76
- VIDEO: Viongozi 11 kitanzini ajali ya moto Morogoro
“Nimepatwa na uchungu mno lakini kwa kuwa umri wangu hauruhusu kuchangia damu, nimeona niwahamasishe vijana ninaofanya nao kazi waje kujitolea damu tuokoe maisha ya wengine,” amesema Mzee Chilo