Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo vya wahamiaji vyaongezeka

34353 Pic+wahamiaji Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Idadi ya vifo vya wahamiaji haramu raia wa Ethiopia imeongezeka kutoka 13 hadi 14 baada ya mmoja kati ya wanne waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro kufariki dunia jana wakati akipatiwa matibabu.

Mganga Mfawidhi hospitali hiyo, Dk Francis Semwene aliliambia Mwananchi jana kuwa, kifo cha mhamiaji huyo kilichotokea juzi saa 1:30 usiku kinaongeza idadi ya vifo na kufikia 14 baada ya awali hospitali hiyo kupokea maiti 13 za wahamiaji wengine.

“Jana saa 10:00 (juzi) jioni tulipokea maiti 13 na majeruhi 13 na kati ya hao wanne hali zao hazikuwa mzuri na mmoja ilipofika kufika saa 1:30 usiku alifariki dunia na kufanya idadi ya vifo vya raia wa Ethiopia kufikia 14 na miili yote imehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali yetu ya mkoa kusubiri taratibu za Serikali,” alisema.

Dk Semwene alisema baada ya wahamiaji hao 13 kufikishwa hospitalini hapo, tisa walipatiwa matibabu na kuruhusiwa na wawili walirejeshwa tena hospitali na kufanya idadi waliolazwa kufikia watano.

Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro, Naibu Kamishna, Saphia Muhindi alisema idara ya uhamiaji inafanya mawasiliano na ubalozi wa Ethiopia nchini kuona kama miili hiyo itazikwa nchini au itasafirishwa kwenda Ethiopia.

Alisema kwamba tayari ubalozi wa Ethiopia umejulishwa na jana walikuwa wakitarajia kumpokea ofisa kutoka ubalozi huo anayefuatilia suala hilo.

“Bado maofisa wa uhamiaji kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola vipo katika uchunguzi wa tukio hili ili kubaini chanzo cha vifo vyao na walioshirikiana nao.



Chanzo: mwananchi.co.tz