Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo vya vya maofisa ununuzi vyaibua madudu Tunduma

Ifopic Data Vifo vya vya maofisa ununuzi vyaibua madudu Tunduma

Fri, 9 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imebaini upungufu katika Halmashauri ya Tunduma mkoani Songwe yaliyosababishwa na maofisa wasio na utaalamu wa ununuzi baada ya vifo vya maofisa ununuzi watatu vilivyotokea mfululizo.

Hayo yamesemwa jana Septemba 8,2022 na Makamu Mwenyekiti wa LAAC, Seleman Zedi mara baada ya kuchambua hesabu za Halmashauri ya Serengeti na Tunduma, zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kwa mwaka unaoishia Juni 31,2021.

Amesema waligundua upungufu katika idara ya ununuzi, ambapo baada ya kumhoji Mkurugenzi wa Halmashauri ya Tunduma alisema kuwa idara hiyo kwa muda mrefu ilikuwa haina ofisa ununuzi.

“Kulikuwa na upungufu kwenye kitengo cha ununuzi, kwamba ofisa aliyekuwepo alifariki, akaletwa mwingine akafariki, akaletwa wa tatu naye akafariki, kwa hiyo ikabidi wachukue mwalimu wa sekondari asimamie ununuzi,” amesema.

Amesema hali hiyo ilisababisha idara hiyo kuwa na makosa mengi ikiwemo wazabuni wasioidhinishwa kupewa zabuni, vifaa kulipwa bila kupokelewa.

“Kamati inampongeza mkurugenzi mpya wa mji wa Tunduma kwa sababu baada ya kuja na kuona kitengo muhimu kama cha ununuzi kinaendeshwa na mwalimu wa kawaida asiye na utaalam wa manunuzi alifanya mawasiliano na Tamisemi (Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa),” amesema.

Advertisement Amesema hivyo Tamisemi ilimtafuta ofisa ununuzi mtaalam kutoka Sumbawanga mkoani Rukwa wakampeleka Tunduma na hivyo tangu alipofika tatizo hilo limekwisha na kitengo hicho kinafanya kazi vizuri sasa.

Aidha, amesema katika Halmashauri ya Serengeti ambayo inazaidi ya kampuni 200, hazilipi ushuru wa huduma wala ushuru unaotokana na mapato ya uwindaji.

“Halmashauri hii wamekuwa wazembe hawafuatilii haya mapato, hii imesababisha halmashauri hii kushindwa kupata mapato yake yanayostahili kuyapata,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live