Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo maporomoko ya Hanang vyafika 69

Mafuriko Hanang 03 At 14.jpeg Vifo maporomoko ya Hanang vyafika 69

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vifo vilivyotokana na maporomoko ya matope kutoka mlima Hanang' mkoani Manyara, vimeongezeka na kufikia 69 baada ya miili minne kupatikana.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi ameyasema hayo leo Jumatano Desemba 6, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari wilayani Hanang'.

Amesema vifo hivyo vimeongezeka na kufikia 69 baada ya miili mingine minne kupatikana leo.

"Kuna miili minne imepatikana leo Jumatano Desemba 6, ambapo kwenye miili hiyo, miwili ni wanawake na wengine wanaume," amesema Matinyi.

Amesema awali kwenye ajali hiyo walikuwa majeruhi 117 ila wengine wamepata ruhusa, mmoja akafariki hivyo idadi yao hivi sasa imepungua na imebaki 45.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live