Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifo Hanang vyafika 89

Hanang Hananggggg Uokoaji.jpeg Vifo Hanang vyafika 89

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Idadi ya vifo vilivyotokana na maporomoko ya matope, mawe na magogo kutoka mlima Hanang, imeongezeka hadi kufika 89.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo Jumatatu Desemba 11, 2023, na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi imesema hadi sasa miili 87 imeshatambuliwa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi ila miwili bado haijatambuliwa.

Maporomoko hayo yaliyotokea alfajiri ya Desemba 3, 2023 na kusababisha majeruhi 139, kati yao 120 walisharuhusiwa na waliobaki hospitali ni 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live