Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vifaa vilivyoibwa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti vyapatikana

76552 Pic+vifaa

Fri, 20 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi wamekamata mifuko 60 ya saruji, vigae 22 na makopo sita ya rangi vinavyodaiwa kuibiwa katika Hospitali ya wilaya hiyo.

Akizungumza leo Ijumaa Septemba 20, 2019 mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu amesema wamekamata vifaa hivyo nyumbani kwa mkazi mmoja mtaa wa Chamoto. Amesema mtu huyo alikamatwa Septemba 18, 2019 na mifuko mitano ya saruji.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,  Juma Hamsini amesema mtuhumiwa  ambaye ni mfanyabiashara  wa mabegi alikutwa amehifadhi vifaa hivyo nyumbani kwake na alishirikiana kuiba na walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi.

"Baada ya kunaswa alikiri kununua vifaa kwa walinzi  na ametumia vifaa hivyo kujengea nyumba yake, juzi amekamatwa na mifuko mitano akisafirisha baada ya kwenda kupekuliwa tukakuta shehena kwake," amesema.

Polisi imesema inawashikilia watu watatu, wakiwemo  walinzi wawili na mnunuzi wa vifaa hivyo, uchunguzi unaendelea kubaini mtandao na thamani ya mali iliyoibwa.

Chanzo: mwananchi.co.tz