Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video ya ajali ya magari manne ndani ya eneo moja Ubungo DSM

Screenshot 2020 07 17 At 09.27.06 660x400.png Ajali Ubungo

Fri, 17 Jul 2020 Chanzo: millardayo.com

Usiku wa kuamkia leo Ubungo Dar es salaam kumetokea ajali zilizohusisha magari manne ndani ya muda mfupi ndani ya eneo moja ambapo gari la kwanza kupata ajali lilikua ni Pickup Mitsubish ambayo inatajwa kuwa kasi ikitokea Kimara kuingia Dar es salaam na papohapo ilisababisha ajali nyingine ya Basi la abiria likitokea Tabora kuingia Dar es salaam, hakuna kifo lakini kuna Mtu mmoja aliyekua nyuma ya pickup amekatika mguu sehemu ya kanyagio.

Ajali ya pili ilitokea dakika chache baadae pembeni ndani ya eneo hilohilo la ajali ya kwanza baada ya gari la mizigo aina ya Dyna kudaiwa kupata pancha na kuacha njia kisha kuparamia gari dogo aina ya Vits ambalo Dereva wake alikua amepaki eneo la tukio, unaweza kutazama hii video hapa chini

MAAJABU YA DUKA LISILO NA MLANGO WA MBAO WALA WA CHUMA NA HAKUNA ANAYETHUBUTU KUIBA KITU, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com