Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vibanda vya machinga vyateketea kwa moto

Moto Chuopic Vibanda vya machinga jirani na hostel za UDSM vyateketea kwa moto

Fri, 12 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeteketeza vibanda vya wafanyabiashara vilivyopo kando ya barabara ya kuelekea katika hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Moto huo ulianza leo Ijumaa Novemba 12,2021 saa 2 asubuhi lakini kikosi cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilifika eneo hilo kuzima moto huo.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Khamis amesema moto umeanzia katika kibanda kimoja cha mama ntilie kabla ya kushika mabanda mengine.

"Banda lililokuwa likifuata ni la kuhifadhia magodoro, ulipoingia ndani ya kibanda hicho uliongezeka na kuwa mkubwa kabla ya kushika banda jingine la kuuza la mbao na kueleke sehemu ya kuosha magari," amesema Khamis.

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Makaburi Kibangu, Moshi Khaftan amesema alipata taarifa ya moto huo ya saa moja na nusu asubuhi na kupiga simu Zimamoto.

Chanzo: mwananchidigital