Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vibanda Soko la Mwananyamala vyavunjwa usiku, wafanyabiashara ni kilio!

Mwananyamala 21 Soko la Mwananyamala

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wafanyabiashara katika soko la Mwananyamala jijini Dar es Salaam, wamelalamika kuvunjiwa vibanda vyao usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Februari 23, 203 bila kupewa taarifa yoyote.



Baadhi ya wafanyabiashara wa soko hilo ambalo ni maarufu kama Soko Mjinga wamesema baada ya vibanda kuvunjwa bidhaa zimechukuliwa na kuwasababishia hasara.

“Jana majira ya saa 5 usiku nilikutana na mtu mmoja akaniambia jamaa wanakuja kuvunja usiku, ikabidi niwajulishe wenzangu kwamba usiku kuna watu wanakuja kuvunja lakini siwezi kuwajua ni akina nani.



“Ilipofika saa 6 usiku, mitaa ya nyuma hapo wale jamaa walikusanyika na wapo wengi sana, wakaja kuvamia huku pamoja na gari za Serikali tatu na difenda za polisi. Niliwauliza polisi kwa nini mnatuvunjia?,” amesema Thomas Robert ambaye ni mfanyabiashara wa nyanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live