Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vibanda 15 vyateketea kwa moto Mafinga

Motoopiic Vibanda Vibanda 15 vyateketea kwa moto Mafinga

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Moto umezuka saa saba usiku wa kuamkia leo Ijumaa Oktoba 21, 2022 pembezoni mwa Soko la Mafinga Mjini Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa na kuteketeza vibanda 15 na mali za wafanyabiashara.

Mmiliki na shuhuda, Mohamed Migila amesema kuwa moto huo ulianza kuwaka usiku na mali nyingi zimeteketea kutokana na shughuli ya uokoaji kuwa mgumu baada ya moto kusambaa kwenye vibanda hivyo.

"Baada ya moto kuwaka, tulifanya jitihada mbalimbali kwa ajili ya kuokoa mali za wafanyabiashara hao lakini hatujafanikiwa baada ya moto kusambaa kwenye vibanda hivyo," amesema Migila.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Iringa, SF Isabela Mbwago amethibisha kutokea kwa moto huku akisema thamani ya mali ambazo zimeteketea bado haijafahamika.

Chanzo: mwanachidigital