Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vibaka waiba koki 50 kwenye mita za maji usiku

Koki Maji Mita Vibaka waiba koki 50 kwenye mita za maji usiku

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa mtaa wa Bigwa Barabarani Manispaa ya Morogoro usiku wa kuamkia tarehe 6 Augosti 2022 wamevamiwa na watu wanaosadikika kuwa ni vibaka na kuibiwa 'Valve' za mita za maji zaidi ya 50 katika mtaa huo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakazi hao wamesema asubuhi ya tarehe 6 waliamka na kukuta maji yanamwagika kwenye mita zao huku mita zikiwa zimefunguliwa na baadhi ya vifaa kuchukuliwa.

Aidha kufuatia tukio hilo wakazi hao walienda kutoa taarifa ofisi ya serikali ya mtaa ili kupata msaada zaidi na ndipo mwenyekiti wa mtaa huo alipotoa taarifa polisi pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa maji safi na maji taka Morogoro-MORUWASA.

Msimamizi wa mradi huo wa maji wa Bigwa kutoka MORUWASA Agapiti Joseph amesema zaidi ya wananachi 50 katika mtaa wa Bigwa Barabarani wameibiwa 'Gate Valve'

Kufuatia tukio hilo Mkurugenzi wa Mamlaka ya usimamizi wa maji safi na maji taka Morogoro - MORUWASA Mhandisi Tamimu Katakweba kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamelazimika kufanya msako katika maduka yanayouza vifaa vya maji na kubaini baadhi ya vifaa ambavyo ni mali ya serikali.

Katika msako huo wamiliki watano wa maduka wamekamatwa kwa upelezi zaidi baada ya kukutwa wakiuza fivaa ambavyo ni mali ya serikali.

Wakati wa msako Katakweba akatumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi kudai lisiti-Satakabadhi ya manunuzi pale wanaponunua vifaa vya bomba.

Bado hadi sasa hasara kamili ya uharifu huo haijatajwa japokuwa katika wizi huo valuvu zilizoibwa ni zile za elfu 15,000 na elfu 25000.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live