Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wajane na wagane wamtembelea Jackline Mengi, wampa neno

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Umoja wa wajane na wagane Tanzania (Tawia) umemtaka Jackline Mengi kuwa mvumilivu katika kipindi hiki anachopitia cha changamoto ikiwa ni miezi michache baada ya kufiwa na mumewe.

Wanachama wa umoja huo leo Jumatatu Agosti 26,2019 wamemtembelea Jackline nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam kumfariji kutokana na msiba wa mmewe, Reginald Mengi uliotokea Mei 2 mwaka 2019.

Mengi alifikwa na mauti akiwa Dubai katika Falme za Kiarabu na mwili wale ulirejeshwa Tanzania Mei 6, 2019 na ulizikwa nyumbani kwao Machame Mei 9, 2019.

Mkurugenzi wa Tawia, Rose Sarwati amemtaka mjane huyo kusimama imara ili maisha yaendelee licha ya kumpoteza mume wake.

“Tumekuja  kukufariji na kukueleza kuwa wenye hali kama yako tuko wengi na tunaishi kwa kufarijiana, unatakiwa kuwa imara ili maisha yaendelee,” amesema

“Tunafahamu mengi yanaibuka na kuzungumzwa ila ifike wakati jamii itambue suala la kifo lipo na tunatakiwa kulikubali,” ameongeza

Pia Soma

Kwa upande wake, Jackline ametoa shukrani zake kwa umoja huo kumtembelea na kumfariji kwani imeleta maana kubwa kwenye maisha yake.

“Sijui hata nianzie wapi, sina mengi ya kusema zaidi ya kushukuru, nimeguswa na upendo kutoka kwa akina mama wenzangu. Tuendelee kupendana na kushirikiana,” amesema

“Nawapa pole na nyie maana najua ninayopitia hata nyie mlipitia tuendelee kupeana moyo, Mungu aendelee kutubariki na ninawashukuru,” amesema Jackline huku akijifuta machozi

Wajane hao walimpatia zawadi ikiwemo vitenge na vikoi ambavyo walivitumia kama ishara ya kumpa joto.

SOMA ZAIDI

> Jacqueline Mengi amshukuru Rais Magufuli

> Jacqueline Mengi: Kwa Mengi sijafuata fedha, bali mapenzi

Chanzo: mwananchi.co.tz