Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Mwenge wazindua miradi 28 mkoani Lindi

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Miradi 28 ya  Sh12.8 bilioni imezinduliwa, kukaguliwa  na kuwekewa mawe ya msingi mkoani Lindi wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema hayo leo Jumatatu  Oktoba 14, 2019 katika kilele cha mbio za Mwenge uliokimbizwa katika halmashauri za mikoa yote ya Tanzania Bara.

Mbio hizo zinahitimishwa mkoani Lindi sambamba na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Zambi amesema kwa kuwa kauli mbiu ya mwaka 2019 inahusu maji ni uhai, Mkoa huo unaendelea kusambaza maji kwa wananchi wake.

“Upatikanaji maji vijijini katika Mkoa wetu ni asilimia 57 na mijini ni asilimia 68, tunaamini  kwa kipindi kilichobaki tunaweza kufika kwa kiwango ambacho kinaelekezwa katika ilani ya uchaguzi ya CCM,” amesema mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi.

Kuhusu mapambano dhidi ya rushwa, Zambi  amesema Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Lindi ilipokea taarifa 249 za rushwa kati ya Julai 2018 na Septemba 2019.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Amesema  kati ya taarifa hizo wamefungua majalada 32 na kuendelea na uchunguzi katika kesi 73 na  kushinda   11.

Chanzo: mwananchi.co.tz