Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Michango ya harusi ilivyotumika kumzika bi harusi mtarajiwa

Video Archive
Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbarali. Kamati ilikuwa na kazi ya kukusanya michango kwa ajili ya kumuaga binti yao (send-off) ili akaungane na mumewe mtarajiwa na kuunda familia moja.

Michango ilipatikana, si haba ilitosha, lakini badala ya kumuaga binti kutoka kwa wazazi wake, ikatumika kumuaga hapa duniani.

Kufuatia vifo vya watu wanne wa familia moja akiwamo bibi harusi mtarajiwa, familia na kamati iliyokuwa ikiratibu sherehe ya kumuaga (send-off party) binti yao ilikubaliana fedha zilizopangwa kutumika kwenye shughuli hiyo, zitumike kwenye mazishi.

Vifo hivyo vilitokana na ajali ya gari iliyotokea alfajiri ya Jumatano iliyopita eneo maarufu kwa jina la Machimbo, Barabara Kuu ya Mbeya-Makambako.

Ajali hiyo ilitokea baada ya gari walilokuwa wakisafiria familia hiyo kutoka nyumbani kwao Chimala wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam kugongwa na gari kubwa aina ya Mitsubishi Fuso ubavuni kwa nyuma kisha kutumbukia mtaroni na kupinduka na watu hao wanne kufariki papo hapo na ndugu wengine wawili kujeruhiwa.

Waliofariki na kuzikwa juzi kwenye makaburi ya Kijiji cha Igumbilo-Chimala mkoani Mbeya ni Diana Mwandunga (28), ambaye alikuwa bibi harusi mtarajiwa na mtoto wa nane kuzaliwa katika familia hiyo.

Pia Soma

Taarifa zaidi Soma Gazeti la Mwananchi la Jumapili Juni 23,2019, Pamoja na kutizama video hii--

Chanzo: mwananchi.co.tz