Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Makonda ashangaa kupewa taarifa potofu za miradi

78100 MAKONDAPIC

Wed, 2 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Takribani wiki moja baada ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kudai kuna watendaji wanaomhujumu na kuahidi kuanza ufuatiliaji, jana alianza kukagua miradi ya maendeleo.

Alitembelea Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-ujenzi wa Soko la Magomeni, Soko la Tandale, ujenzi wa Mto Ng’ombe na baadhi ya barabara ikiwamo ya Sinza Makaburini- ambako alisema amesikitishwa na baadhi ya miradi kutoanza kutekelezwa tofauti na taarifa aliyopokea.

Akizungumza baada ya kutembelea mradi wa mto huo alisema inasikitisha kuona taarifa aliyopewa kuhusu ujenzi huo hailingani na uhalisia.

“Kuna baadhi ya taarifa zipo sahihi nyingine hazipo sawa. Bado kuna watu hawataki kutekeleza wajibu wao, hawafanyi kazi, “ alisema Makonda.

“Mradi huu haujaanza kujengwa wakati mkataba ulisainiwa tangu mwezi wa sita.”

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz