Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza miradi yote katika mkoa huo ikamilike kabla ya uchaguzi mkuu ujao 2020.
Makonda ametoa kauli hiyo leo Jumatano Septemba 25,2019 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao cha uchambuzi wa miradi ya maendeleo iliyokwama katika jiji hilo.
Wakuu wa wilaya za Ubungo, Kinondoni, Ilala, Temeke, Kigamboni pamoja na Jiji hilo wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa miradi iliyokwama na iliyokamilika, yenye thamani ya takribani Sh3trilioni.
"Ukiangalia kwa ujumla ni kama miradi yote imekamilika kwa asilimia 75 hadi 80, wako wanaofanya vizuri lakini wengine ukienda field, hadi kufikia Mei mwakani miradi yote iwe imekamilika, " amesema Makonda.
"Tujenge timu ya matokeo chanya, kila mmoja atambue upungufu aliyonayo katika nafasi yake, aibu tuliyoipata tusipate tena."
Mkutano huo umehusisha Wakurugenzi, Wakuu wa wilaya, watendaji, wakandarasi, Maofisa wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) pamoja na viongozi wa CCM ngazi ya wilaya na mkoa.
Habari zinazohusiana na hii
- Magufuli ahoji utendaji kazi wa viongozi Dar
- Magufuli ashauri kuachiwa mahabusu wa uhujumu uchumi
- Magufuli ateua viongozi wa tume ya haki za binadamu
- Magufuli azungumzia ugumu anaokutana nao katika kuteua, kutengua