Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Makandarasi wakamatwa na polisi kwa agizo la Makonda

Video Archive
Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mkandarasi anayejenga  barabara ya Banana-Kitunda  wa kampuni ya  Nyanza na mwingine anayejenga daraja la mto Ng’ombe wamekamatwa na polisi kwa agizo la mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Wamekamatwa kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 24, 2019 Katibu tawala Mkoa wa Dar es Salaam,  Abubakar Kunenge amesema licha ya kulipwa fedha lakini makandarasi hao wameshindwa kutekeleza kazi waliyopewa.

Hivi karibuni Makonda aliagiza makandarasi hao kumaliza ujenzi ndani ya siku tano, endapo hawatafanya hivyo hatua zitachukuliwa.

“Kwa hiyo waliokamatwa leo ni makandarasi  wanaojenga  barabara ya Kivule iliyopo Ukonga. Serikali imetenga Sh32 bilioni na tayari amelipwa Sh4.8 bilioni lakini maendeleo ya mradi yanasuasua,” amesema Kunenge.

Kuhusuu ujenzi wa daraja, amesema tayari mkandarasi amekabidhiwa zaidi ya Sh800 milioni lakini ameshindwa kutekeleza mradi kwa wakati.

Pia Soma

Advertisement

Amesema sheria ya tawala za mikoa inampa mamlaka mkuu wa Mkoa kuwakamata wenye dalili za kuhatarisha maisha.

Amesema kucheleweshwa ka miradi hiyo kunalenga kuwachonganisha wananchi na Serikali, “kukamatwa kwao iwe fundisho kwa makandarasi wengine wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz