Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Majeruhi 17 wa ajali ya treni waruhusiwa, watatu hali zao bado

Video Archive
Tue, 18 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Majeruhi wanane kati 25 wa ajali ya treni ya abiria iliyokuwa ikitokea Kigoma kwenda Dar es Salaam bado wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumanne Juni 18 2019, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk James Charles amesema waliwapokea majeruhi hao saa 5.45 jana Jumatatu usiku ambapo wengi wao walikuwa wamepata mshtuko.

“Majeruhi nane bado wanaendelea na matibabu na 17 tuliwaruhusu baada ya kupatiwa matibabu. Hali zao zinaendelea vizuri,” amesema.

Naye Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk Abdul Pumzi amesema majeruhi watatu kati ya hao watahitaji kukaa zaidi hospitalini kwa ajili ya matibabu.

“Majeruhi watatu watahitaji kukaa hospitali zaidi na wawili wamevunjika mfupa, mwingine majeraha ya kifua,” amesema.

Amesema majeruhi wanaohitaji huduma ya upasuaji watafanyiwa upasuaji ndani ya siku mbili.

Habari zinazohusiana na hii

Ajali hiyo ilihusisha lori lililoigonga treni ya abiria karibu na Stesheni ya Dodoma.

Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachoendelea

Chanzo: mwananchi.co.tz