Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Kamati yacharaza bakora wananchi wenye madumu

Video Archive
Mon, 13 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Kamati ya ulinzi na usalama mtaa ya Madaganya kata ya Mindu wamewatawanya wananchi huku wakilazimika kutumia bakora baada ya kutaka kulivamia lori la mafuta lililopinduka.

Kazi hiyo iliyodumu kwa dakika 40 ilisababishwa na lori la mafuta kupinduka alfajiri ya jana katika barabara ya Morogoro-Iringa.

Akizungumza jana mjini hapa, mwenyekiti wa mtaa ya Madaganya, Ahmad Disembe alisema kamati ya ulinzi ililazimika kufanya kazi ya ziada ya kuwatawanya wananchi ambao baadhi yao walishika madumu matupu kwenda kukinga mafuta.

Disembe alisema baada ya kupata taarifa ya uwapo wa ajali hiyo, wananchi walikusanyika haraka baadhi wakiwa na madumu tupu.

“Ajali imetokea saa 10:00 alfajiri ya leo (jana) niliwakusanya kamati ya ulinzi na kuimarisha ulinzi eneo la tukio, lakini tulikumbana na changamoto ya watu wenye madumu tupu waliokuwa wakikimbilia kufungua tangi kukinga mafuta,” alisema.

Aalisema walilazimika kutumia nguvu kabla ya polisi kufika na kudhibiti hali na na kwamba, wangeshindwa yangetokea maafa kama ya Agosti 8, mwaka jana ambayo watu 100 walifariki eneo la Msamvu.

Pia Soma

Advertisement

Dereva asimilia

Dereva wa lori la mafuta aina ya Scania, Amri Juma alisema ajali hiyo ilitokea baada ya dereva mwenzake wa lori lililobeba mahindi kumfuata upande wake.

Juma alisema hakuna madhara yaliyotokea kwa binadamu kwani alifanikiwa kutoka ndani ya gari na kukaa pembeni.

“Baada ya gari langu kupinduka nilitoka salama ndani ya gari na mtu wa kwanza kufika eneo la tukio ni mwenyekiti wa mtaa, tuliwatahadharisha wananchi waliokuwa wanasogea kufungua tangi ili wakinge mafuta,” alisema Juma.

Alisema aliwataka wananchi kukaa mbali na lori hilo kwani lina petroli ambayo ni hatari kwa usalama wao.

“Nawashukuru walinielewa muda mfupi watu wa kamati ya ulinzi na usalama ya mtaa walifika kisha polisi nao wakaja.” alisema.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea ajali iliyosabishwa magari mawili kugongana.

Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea eneo la Madaganya baada ya lori aina ya Scania lenye tela mali ya kampuni ya Dani Kinyunyu, kugongana na lori aina ya Scania tengi la mafuta.

“Lori la mafuta lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Zambia liligongana na lingine la mahindi likitokea Makambako kuelekea Dar es Salaam,” alisema.

Chanzo: mwananchi.co.tz