Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Jokate alivyotua kwa wazee wa kupapasa

Video Archive
Thu, 23 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Pwani. Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, Jokate Mwegelo ni miongoni mwa wageni ambao wamejitokeza kwenye Uwanja wa Mabatini kwa ajili ya kuishuhudia Ruvu Shooting ikitupa karata yake ya kwanza ya  Ligi Kuu Bara  dhidi ya Ndanda FC.

Jokate ambaye ni mwanamitindo wa zamani  ameingia katika uwanja huu maarufu kwa jina la machinjioni muda mchache baada ya mechi kuanza.

Alipoingia tu, aliwasalimia mashabiki wa Ruvu Shooting ambao wamejitokeza kwa wingi na kuketi upande wa VIP pamoja na wenyeji wake.

Hii ni mara ya kwanza kwa mkuu huyo wa Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani kuja kuishuhudia Ruvu Shooting ikicheza katika uwanja wao wa nyumbani.

Ruvu ndiyo timu pekee inayoshiriki Ligi Kuu Bara kutoka katika Mkoa huo wa Pwani.

Klabu ya Ruvu Shooting ni maarufu kwa jina la wazee wa kupapasa.

Chanzo: mwananchi.co.tz