Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Hapi awageukia wanaomhujumu Rais

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amewashukia baadhi ya viongozi wastaafu walioamua kumhujumu Rais wa Tanzania John Magufuli.

Hapi amesema hayo leo Julai 21 ofisini kwake wakati akizungumza na wanahabari kuhusu kuibuka kwa mijadala mbalimbali ndani ya nchi inayoigusa Serikali inayoongozwa Magufuli.

Hapi amesema mijadala hiyo imewahusisha baadhi ya viongozi hao wastaafu waliotumikia nchi kwa kipindi kirefu.

“Jitihada za wastaafu hao zimelenga kupeleka mashambulizi kwa Rais wetu, lakini zikiwa na maana ya kuligawa Taifa letu; ni mambo ambayo sote tumeyashuhudia siku za hivi karibuni,” amesema.

 “Na mimi kama mkuu wa mkoa niliyeteuliwa na Rais Magufuli niliyekula kiapo kutetea katiba na kulinda umoja na  mshikamano wa nchi siwezi kukaa kimya.

“Mimi kama mkuu wa mkoa niliyelelewa kwenye chama na bahati mbaya au nzuri wazee hawa ambao wamekuwa wakitoa nyaraka na matamko mbalimbali ni wazee ambao tumekuwa kwenye chama tukiwaheshimu sana kama viongozi wetu ndani ya chama,”amesema.

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz