Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Halaiki yawa kivutio kumbukumbu kifo cha mwalimu Nyerere

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wanafunzi waliocheza halaiki katika kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha mwalimu Julius Nyerere wamekuwa kivutio kwa kutengeneza maumbo ya ramani mbalimbali.

Maadhimisho hayo yanayofanyika sambamba na kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru  katika uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Wanafunzi hao wameunda maumbo ya ramani  ya Tanzania, Mkoa wa Lindi, Mwenge wa Uhuru na Bendera ya Taifa pamoja na umbo la  mjusi mkubwa wa Tanzania aliyepo nchini Ujerumani.

Rais wa Tanzania, John Magufuli ndio mgeni rasmi katika maadhimisho hayo.

‘Tumejitahidi, tunatekeleza, awamu ya tano 2015-2020,’ ni baadhi ya maneno yaliyoumbwa na wanafunzi hao.

Wanafunzi hao waliovaa mavazi meupe  walitembea kama askari kuelekea mbele ya jukwaa wakiwa wameshika njiwa ambao baadaye waliwaachia na kuruka.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz