Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Daraja linalounganisha Handeni na Kilindi lasombwa na maji

Video Archive
Fri, 25 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Daraja linalounganisha Wilaya ya Handeni na Kilindi mkoani Tanga katika eneo la Nderema limesombwa na maji leo asubuhi Oktoba 25, 2019  kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Kusombwa na daraja hilo kumesababisha magari yanayofanya safari kati ya wilaya hizo mbili kukwama na mengine kusaka njia mbadala kupitia Msente mpaka Kideleko ambazo pia zinapitika kwa tabu kutokana na mvua.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Watumiaji wa barabara Korogwe-Segera kwenda mikoa ya Kaskazini wanataarifiwa kuwa daraja la Mandela limejaa, halipitiki, hivyo njia hiyo imefungwa tena, hivyo wanaoelekea na kuja Tanga na Dar es Salaam wanashauriwa kuipitia Handeni mjini

Chanzo: mwananchi.co.tz