Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Abainika amekufa ndani ya nyumba yake baada ya siku 4

Video Archive
Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Neema Kavishe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 33, amebainika kupoteza maisha zaidi ya siku nne nyuma ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi.

Neema alikuwa mpangaji wa nyumba za Shirika la Nyuma la Taifa (NHC) zilizopo Shekilango, sehemu ambayo imetajwa kuwa alihamia kwa zaidi ya miaka minne iliyopita.

Taarifa za kufariki kwake zimejulikana leo Jumatano, Juni 19, 2019, baada ya majirani zake kuhisi harufu iliyokuwa ikitokea ndani ya nyumba yake huku nzi wakizagaa katika maeneo ya madirisha yake.

Kwa mujibu wa wa Daktari wa kituo cha Afya Mbezi, Miriam Cheche ambaye ni jirani, tangu jana usiku alikuwa akisikia harufu ikitokea upande huo, jambo lililomfanya ahisi ni taka zilizokusanywa karibu na eneo hilo.

“Lakini asubuhi wakati najiandaa kuoga, nilisema hapana, hii ni harufu ya mtu kwa sababu mimi ni daktari na ninajua harufu hizo, tulitoa taarifa kituo cha polisi na mlango ukavunjwa tukamkuta akiwa tayari ameanza kuharibika,” amesema Miriam.

Uongozi wa kituo cha Polisi Urafiki ulisema mwili umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Pia Soma

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz