Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzinduzi safari ya treni Tanga-Kilimanjaro watajwa kuleta neema

67609 Treni+pic

Sat, 20 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella amesema uzinduzi wa safari ya treni ya mizigo kutoka Tanga hadi Moshi mkoani Kilimanjaro utafungua fursa mpya za uwekezaji katika Mikoa hiyo.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumamosi Julai 20, 2019 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Shigela amesema treni hiyo mpya itapunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kutoka Tanga hadi Kilimanjaro.

"Tunamshukuru  Rais Magufuli (John- Rais wa Tanzania) kwa kuhakikisha safari za treni  zinafufuliwa maana zitasaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo ikiwemo  saruji inayozalishwa kwa wingi kutoka Tanga kuja Kilimanjaro, "amesema.

Kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira  amesema uzinduzi  wa treni hiyo ni tukio la kihistoria nchini.

 

Pia Soma

 

Chanzo: mwananchi.co.tz