Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uzalishaji maji Ruvu warejea katika hali yake

Ruvu Maji Mjai Uzalishaji maji Ruvu warejea katika hali yake

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kazi ya Marekebisho ya Pampu ya kusukuma maji katika mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Chini imekamilika.

Marekebisho haya yalisababisha upungufu wa uzalishaji maji kutoka lita milioni 270 hadi lita milioni 220 kwa siku.

Matengenezo yamekamilika leo, February 26, 2024 na kurudisha hali ya uzalishaji katika kawaida yake ya ujazo wa lita milioni 270 kwa siku.

Maeneo yafuatayo yataanza kupata huduma ya maji kwa msukumo mzuri :- Bagamoyo, Mapinga, Mabwepande, Bunju, Tegeta, Mbweni, Boko, Salasala, Goba, Mivumoni, Kawe, Lugalo, Makongo, Chuo, Kikuu, Mwenge, Kijitonyama, Mikocheni, Msasani, Oysterbay, Masaaki, Mwananyamala, Kinondoni, Magomeni, Kigogo, Chang'ombe, Keko, Kurasini, Kigamboni, Airport, Kiwalani, Buguruni, Vingunguti, Ilala na Katikati ya Jiji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live