Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwasa kupandisha bei ya maji Tanga

9897 Pic+bei+maji TZWeb

Sun, 24 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Uwasa) imewasilisha mapendekezo ya kupandisha bei ya ankara ya maji kwa asilimia 38.6 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/19 na asilimia 16.9 mwaka 2019/20.

Mapendekezo hayo yanatokana na mamlaka hiyo kuhitaji Sh41.28 bilioni ili kufanikisha mipango yake.

Meneja wa Tanga-Uwasa, Fares Alen alisema hayo jana katika mkutano wa wadau wa maji uliofanyika chini ya uratibu wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Maji na Nishati (EWURA CCC).

Alisema nyongeza hiyo ya bei itaisaidia mamlaka kutekeleza vipaumbele vyake ilivyojiwekea ikiwamo kuwaunganisha wateja wapya 2,000 wa majisafi kila mwaka, majitaka 50, kununua vitendea kazi na kukarabati majengo.

“Tunapendekeza bei ya majisafi ipande kutoka Sh28.92 inayolipwa sasa kwa ndoo moja ya lita 20 hadi kufikia Sh40.00 kipindi cha mwaka 2018/19 na Sh46.89 mwaka 2019/20 wakati bei ya majitaka itoke Sh400 hadi kufikia Sh568.00 mwaka 2018/19 na Sh626.00 kwa mwaka 2019/20,” alisema Alen.

Watumiaji wa maji waliiomba Tanga-Uwasa kuboresha baadhi ya huduma zake kama kuwaunganishia maji wateja wapya na kuimarisha mfumo wa upokeaji wa malipo.

Meneja wa Ewura, Kanda ya Mashariki, Nyirabu Msila aliwaomba watumiaji wa maji kuipa muda Tanga-Uwasa ifanye maboresho baadhi ya maeneo ili iweze kuwasilisha tena mapendekezo ya nyongeza hiyo ya bei ya maji.

Chanzo: mwananchi.co.tz