Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa ndege Musoma kukamilika 2022

WizarayaujenzinauchukuzipCXsUvl8NEBn1 1080x640 Uwanja wa ndege Musoma kukamilika 2022

Mon, 20 Dec 2021 Chanzo: dar24.com

Imeelezwa kuwa pindi Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma utakapokamilika utafungua usafiri wa anga kwa Mkoa wa Mara na kuwa kiunganishi kikubwa na mikoa jirani ya Kanda ya Ziwa.

Hayo yamesemwa mkoani Mara na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, wakati akikagua ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege kwa kiwango cha lami wenye urefu wa kilometa 1.75 ambapo utaruhusu ndege za Q400 Bombadier kutua kwa urahisi kiwanjani hapo.

Prof. Mbarawa amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Musoma unaogharimu kiasi cha shilingi bilioni 35.047 na mkandarasi anayetelekeza mradi huo ni Beijing Construction Company Limited ambapo kazi zinaendelea kwa kasi.

“Kiwanja cha Ndege cha Musoma kitakapokamilika kitafungua anga kwa kiasi kikubwa na kukuza uchumi wa mkoa wa Mara na mikoa jirani”, amesema Prof. Mbarawa.

Kuhusu suala la fidia, Waziri Mbarawa amesema Serikali imekwisha lipa fidia kiasi cha shilingi Bilioni 3.955 kwa wananchi waliopisha ujenzi huo.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe, ameeleza kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Disemba 2022 na unahusisha barabara ya kuruka na kutua ndege, barabara ya maegesho ya ndege, jengo la kuongezea ndege na jengo la zima moto.

Chanzo: dar24.com