Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Ndege wa Bukoba wafunguliwa tena

Uwanja Wa Ndege Bukoba Uwanja wa Ndege wa Bukoba wafunguliwa tena

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uwanja wa ndege wa Bukoba Kaskazini - Magharibi mwa Tanzania umefunguliwa tena kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya watu 19 na majeruhi 24.

Ndege hiyo ya abiria ilianguka katika Ziwa Victoria ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja huo Jumapili.

Afisa utawala katika mji huo ameiambia BBC kwamba ndege ya kwanza ya abiria inatarajiwa kutua kwenye uwanja wa Bukoba leo Alhamisi.

Washauri wa kiufundi kutoka kwa watengenezaji wa ndege, ATR, wameanzisha uchunguzi kuhusu ajali hiyo. Wataalamu wa Ufaransa wa usalama wa safari za ndege pia wamepelekwa nchini humo.

Ndege hiyo ilikuwa ni ya kampuni ya Precision Air - kampuni kubwa zaidi ya kibinafsi ya safari za ndege za abiria nchini Tanzania. Imekuwa ikiendesha safari zake kutoka Dare es salaam - Bukoba tangu mwaka 1994.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live