Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa Ndege Tabora kuwa na sura ya kimataifa

892514449014ded2cc2b0fec4f180788 Uwanja wa Ndege Tabora kuwa na sura ya kimataifa

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Tawi la Tabora imetakiwa kuwasiliana na mkandarasi ambaye ni Kampuni ya M/S Beijing Construction Engineering Group Co. Ltd (BCEG) China ili aweze kuanza maboresho ya ya Uwanja wa Ndege wa Tabora kwa ajili ya kuuweka katika sura ya kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Philemon Sengati wakati wa ziara yake ya kuona maandalizi ya ukarabari na upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Tabora.

Alisema toka Oktoba mwaka huu, serikali imeshatoa sh bilioni 27 kwa ajili ya uboreshaji wa Uwanja wa Ndege Tabora ambapo miongoni mwa shughuli zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa jengo la abiria, maegesho ya magari na uzio wa usalama kuzungunguka eneo la uwanja huo na mnara wa kuongozea ndege.

Dk Sengati alisema uwanja huo ni vema ukakamilika kwa wakati kwa sababu utasaidia kuinua sekta mbalimbali za uchumi ikiwemo kuvutia wawekezaji na watalii ambao wanahitaji kutembelea hifadhi za taifa zinazopatikana mkoani Tabora.

Alisema ni vema mamlaka hiyo ikandaa mpango wa kuongeza eneo la uwanja huo ambalo litasaidia siku ya baadaye kuendeleza uboreshaji wa miundombinu zaidi.

Dk Sengati alisema kuna wananchi wameanza kujenga nyumba katika maeneo yanayokaribiana na uwanja huo ni vema wakachukua hatua mapema ili kuepuka kuzalisha gharama kubwa ya kulipa fidia pindi watakapohitaji maeneo hayo kwa ajili ya kuongeza miundombinu ya uwanja.

Naye Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Tabora, Godfrey Kaaya alisema jengo la abiria wanalokusudia kujenga litakuwa na uwezo wa kuchukua abiria 250,000 kwa mwaka hadi kufikia mwaka 2035.

Aliongeza kuwa mradi wa uboreshaji uwanja wa Tabora utakuwa na ujenzi wa barabara za magari na maegesho ya magari na kujenga uzio wa usalama kuzunguka eneo la uwanja huo lenye ukubwa wa hekta 881.14.

Kaaya alisema kukamilika kwa uboreshaji huo kutaongeza uwezo wa Uwanja wa Tabora wa kuhudumia abira kutoka 100 wa sasa hadi kufikia 500 kwa wakati mmoja.

Alitaja faida nyingine ni kuongezeka kwa ndege za abiria na mizigo na kufunguka kwa Mkoa wa Tabora katika miundombinu.

Chanzo: habarileo.co.tz