Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uvamizi waporomosha Tanzania vivutio vya asili

65672 Pic+uvamizi

Fri, 5 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Tanzania imeshuka kutoka nafasi ya pili hadi ya nane kwa kuwa na vivutio vya asili vya utalii duniani.

Mshauri wa  uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa), Ibrahim Mussa ametaja uvamizi na shughuli za kibinadamu katika maeneo ya hifadhi kuwa miongoni mwa sababu za anguko hilo.

Akitoa mada leo Julai 5, 2019 kwenye mkutano wa Wahariri, Waandishi waandamizi na Tanapa unaoendelea jijini Mwanza, Tanzania,  Mussa amesema takwimu hizo ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka 2018 baada ya utafiti uliofanyika mwaka 2017.

“Kipindi kilichopita tulikuwa nafasi ya pili nyuma ya Brazili; lakini hivi sasa tumeshuka,” amesema Mussa.

Hata hivyo, Tanzania ni kinara kwa bei na gharama nafuu katika sekta ya utalii kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) kulinganisha na vivutio wanavyovishuhudia  wanapotembelea nchini.

Chanzo: mwananchi.co.tz