Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utoaji wa chanjo wazorota Mkoani Tanga

CHANJOOO Chanjo

Thu, 23 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Jonathan Budenu amesema katika zoezi la utowaji chanjo ya virusi vya Corona walilenga watu 139,000 lakini hadi sasa wametoa chanjo kwa watu 10,939 sawa na 31%.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amewataka Wataalamu wa Afya kuacha Siasa katika Ugonjwa huo na kuwaelimisha watu ili waweze kujitokeza kupata chanjo.

Malima amesema "Wataalamu wa Afya kama mmeweza kuhamasisha Wazazi kuhusu umuhimu wa kuchanja watoto wachanga basi nendeni mkahamasishe watu umuhimu wa chanjo ili kuendelea kujikinga na Ugonjwa wa Corona".

Hata hivyo, muamko wa wananchi kupata chanjo katika maeneo mbalimbali nchini bado ni mdogo kutokana na kuenea kwa habari potofu kuhusu chanjo ya Corona.

Hivyo serikali na vyomba vya habari wanapaswa kuongeza jitahada za kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kupata chanjo ili waweze kuimarisha kinga za mwili na kupunguza maambukizi ya virusi hivyo nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live