Mrembo aliyejulikana kwa jina la Mariam Bruno (34), pichani kulia mkazi wa Mtaa wa Olkereian Kata ya Olasiti Jijini Arusha amefariki Dunia katika mazingira ya kutatanisha.
Tukio hilo limetokea juzi Jumatatu, baada ya siku kupigiwa simu na rafiki yake aitwaye Anitha amfuate maeneo ya baa ya Amarula iliyopo mtaa wa kambi ya Fisi kata ya Ngarenaro ambapo kuanzia hapo hakuwasiliana tena na ndugu zake mpaka pale walipopigiwa simu na polisi kwamba binti huyo amefariki yuko mochwari.
Ndugu hao wameelezwa kuwa Mariam alikosa hewa katika moja ya chumba katika baa hiyo jambo ambalo wameomba upelelezi kufanyika kwa haki ili kujua chanzo huku wakilalamika kuwa aliyempigia simu siku hiyo rafki yake huyo yuko mtaani na hajakamatwa bado na wamesema kuwa hawatazika mpaka wapate ukweli wa tukio zima.
Ndugu hao wamedai kuwa baada ya kuonyeshwa mwili wa marehemu ukiwa na damu huku ukiwa umevimba wote jambo ambalo limewapa wasiwasi na kuzitaka mamlaka husika kufanya uchunguzi ili wajue chanzo cha kifo cha ndugu yao.
Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo zitakujia.....