Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Utata familia ikichomewa nyumba mara ya pili...

Nyumba Kuchomaaaa (600 X 344) Utata familia ikichomewa nyumba mara ya pili...

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utata umeibuka katika kijiji cha Engikaret kilichopo Loliondo mkoani Arusha baada ya familia moja yenye watu 11 kukumbwa na dhahama ya nyumba zake kuchomwa moto mara mbili mfululizo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amekiri kufahamu tukio hilo na kusema vyombo vya ulinzi na usalama tayari vimeanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo.

Familia hiyo ilikumbwa na dhahama ya nyumba kuchomwa moto Desemba 29, 2023. Tukio kama hilo pia lilitokea Januari 26, mwaka huu. Wazee wa kimila wa jamii ya kimasai - Laigwanani wameungana kwa ajili ya kutoa msaada wa vyakula, maji, nguo, na vyombo vya kupikia.

Hata hivyo, taarifa ambazo bado hazijathibitishwa na mamlaka zinadai kuwa matukio hayo yametendwa na wananchi wa Kijiji jirani cha Losinoni kilichopo wilaya ya Arumeru mkoani Arusha. Kisa kimetajwa kuwa ni ugomvi wa mpaka kati ya familia hizo za Arumeru na Longido.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live